fbpx
Skip to content

2016 press release

Read in:

Tuzo ya Mazingira ya Goldman inatoa heshima kwa Mabingwa sita wa Mazingira

Tuzo inakwenda kwa wanaharakati kutoka Tanzania, Cambodia, Slovakia, Peru, Pwetoriko, Marekani

SAN FRANCISCO, Aprili 18, 2016 – Taasisi ya Misingi ya Kimazingira ya Goldman leo ilitangaza mpokeaji wa sita wa Tuzo ya Mazingira ya Goldman 2016, Tuzo kubwa zaidi duniani kwa ajili ya wanaharakati wa mazingira wa ngazi ya chini. Tuzo hizi hutolewa kila mwaka kwa mashujaa wa mazingira kutoka kila moja ya kanda za mabara sita ya dunia ambazo hayajakaliwa, Tuzo za Goldman inatambua wanaharakati wa ngazi ya chini wasiokuwa na woga kwa ajili ya mafanikio makubwa katika kulinda mazingira na jamii zao.

Msindi atatunukiwa Tuzo katika mwaliko wa sherehe tu leo saa 5:30 jioni. San Francisco Opera House (tukio hili linaoneshwa moja kwa moja katika mtandao kupitia www.goldmanprize.org/ceremony). Sherehe katika  Jengo la Ronald Reagan na International Trade Center Washington, DC itafuatia Jumatano, Aprili 20 saa 7:30 Jioni.

Washindi wa mwaka huu ni:

EDWARD LOURE, wa Tanzania
Edward Loure aliongoza chama kilicho anzisha mtazamo ambao ulitoa hati miliki za ardhi kwa jamii – badala ya watu binafsi – za wafugaji na wawindaji – walioko mshariki mwa Tanzania, kuhakikisha usimamizi wa mazingira ya ardhi yao kwaajili ya vizazi vijavyo.

LENG OUCH, wa Cambodia
Katika moja ya nchi hatari zaidi duniani kwa wanaharakati wa kimazingira, Leng Ouch alipita chini kwa chini kukusanya taarifa za uvunaji haramu ndani ya Cambodia na kuziweka wazi rushwa inayowaibia  ardhi zao jamii za vijijini, jambo lililosababisha serikali kufuta umiliki mkubwa wa ardhi.

ZUZANA CAPUTOVA, wa Slovakia
Mwanasheria anayejali maslahi ya umma na mama wa watoto wawili, Zuzana Caputova ikiongoza kampeni yenye mafanikio ambayo ilifunga dampo la taka za sumu ambalo lilikuwa linatia sumu katika ardhi, hewa na maji katika jamii yake, kuweka historia kwa umma kushiriki baada ya ukomunisti wa Slovakia.

LUIS JORGE RIVERA HERRERA, wa Puerto Rico
Luis Jorge Rivera Herrera alisaidia kuongoza kampeni ya mafanikio ya kuanzisha hifadhi ya asili Kaskazini mwa korido la kiuchumi la Puerto Rico – maeneo muhimu kwajili ya matagio ya Kobe wa baharini wenye ngozi walioko katika hatari ya kupotea -na kulinda urithi wa asili wa kisiwa kutokana athari za maendeleo.

DESTINY WATFORD, wa United States
Katika jamii  ambayo haki zake za kimazingira zimeshabanwa kutengeneza nafasi kwaajili ya viwanda vikubwa, Destiny Watford aliwahamasisha wakaazi wa jirani na Baltimore kushinda mipango ya kujenga kiwanda cha kikubwa kitaifa cha uchomaji umbali wa chini ya maili moja kutoka katika shule yake.

MÁXIMA ACUÑA, wa Peru
Mkulima wa kujikimu katika Nyanda za juu kaskazini za Peru, Máxima Acuña alisimama kwa ajili ya haki yake ya kuishi  kwa amani kwa kutegemea ardhi yake, Mali yake ya iliyokuwa inatakiwa na wachimaji wa madini Newmont na Buenaventura, iliyosaidia kuweka machimbo ya Conga nje ya maeneo muhimu ya maji.

Kuhusu Tuzo za Mazingira za Goldman:
Tuzo za mazingira za Goldman zilianzishwa mwaka 1989 na marehemu kiongozi wa kiraiabwana San Francisco na  wahisani Richard na Rhoda Goldman Mshindi wa tuzo za mazingira za Goldman huchaguliwa na wazee wa baraza la kimataifa kutoka katika uteuzi wa siri unaowasilishwa na taasisi za mtandano wa mazingira duniani na watu binafsi. Kwa taarifa zaidi kuhusu Tuzo na washindi waliopita tembelea: www.goldmanprize.org.

# # #