fbpx
Skip to content

2015 press release

Read in:

Goldman Environmental Prize Imewatuza Mashujaa Sita wa Mazingira

2015 wapokeaji kutoka nchini Kenya, Myanmar, Uskoti, Haiti, Kanada, na Honduras

SAN FRANCISCO, Aprili 20, 2015 — Shirika la Goldman la Mazingira leo imetangaza wapokezi sita wa 2015 wa Tuzo ya Goldman ya Mazingira, tuzo kubwa ulimwenguni ya wanaharakati wa ngazi ya chini ya mazingira.

Hutuzwa kila mwaka kwa mashujaa wa mazingira kutoka kwa kila moja ya maeneo sita ya bara yenye wenyeji, Tuzo ya Goldman hutambua wanaharakati mashujaa wa ngazi ya chini wanaofanya kazi dhidi ya matatizo yote ya kulinda mazingira na jumuia zao.
Wao mara nyingi hufanya kazi katika nchi ambapo vurugu na vitisho vya kifo dhidi ya watetezi wa mazingira iko juu, kama ilivyoandikwa  katika ripoti kutoka Global Witness iliyotolewa leo.

Washindi watapewa  Tuzo kwa shehere ya mwaliko-tu siku ya Jumatatu Aprili 20 saa 11:30 alasiri katika Jumba la San Francisco Opera. Sherehe katika Jengo la Ronald Reagan na Kituo cha KImataifa cha Biashara katika Washington, DC itafuata siku ya  Jumatano Aprili tarehe 22 saa 1:30 usiku.

Washindi wa mwaka huu ni:

PHYLLIS OMIDO, Kenya
Baada ya kugundua maziwa yake mwenyewe ya matiti ilikuwa inamfanya mtoto wake kuwa mgonjwa — na kutambua mtoto wake hakuwa mwenye aliyekuwa akiteseka tu kutoka kwa sumu ya risasi —Phyllis Omido alikusanya jumuia huko Mombasa ili kufunga kiwanga cha kuyeyusha madini ambayo ilikuwa inawahatarisha watu kwa kemikali hatari.

MYINT ZAW, Myanmar
Alikabiliwa na uchunguzi nzito wa serikali na kupewa vikwazo kwa matumizi ya zana kama vile barua pepe au mtandao wa, Myint Zaw alizindua harakati ya taifa ambayo ilifaulu  kusimamishwa ujenzi wa Bwawa la Myitsone kwenye Mto Irrawaddy  uliothaminiwa na Myanmar.

HOWARD WOOD, Uskoti
Howard Wood aliongoza kampeni ambayo ilianzisha eneo la kwanza – Bahari lililojengwa nchini Uskoti, na kuwapa wananchi sauti katika mjadala ambao umekuwa unaongozwa na sekta ya biashara ya uvuvi.

JEAN WIENER, Haiti
Katika nchi inayosumbuliwa na umaskini uliokithiri na migogoro ya kisiasa, Jean Wiener aliongozwa juhudi za jamii kuanzisha Maeneo ya kwanza ya Bahari Yaliyohifadhiwa kwa Kuwawezesha Wanahaiti kuona thamani za muda mrefu katika kuendeleza kusimamia uvuvi na misitu ya mikoko.

MARILYN BAPTISTE, Kanada
Chifu wa zamani wa Xeni Gwet katika Taifa la Kwanza, Marilyn Baptiste
aliongozwa jumuia yake katika kuwashinda moja ya mapendekezo ya migodi ya dhahabu na shaba  nchini British Columbia ambayo ingeharibu Ziwa la Samaki Lake—chanzo cha utambuzi wa dini na kujikimu kwa watu wa Xeni Gwet’in.

BERTA CÁCERES, Honduras
Katika nchi iliyo na ongezeko la ukiukaji wa ushirikiano wa kiuchumi kukosekana kwa usawa na haki za binadamu, Berta Cáceres aliwakusanya wenyeji asili wa Lenca wa nchi ya Honduras na kufanya kampeni ya mashinani ambayo ilifaulu kushinikiza wajenzi wakuu wa bwawa duniani kuondoka kwa Bwawa la Agua Zarca.

Kuhusu Goldman Environmental Prize
Goldman Environmental Prize ilianzishwa mwaka 1989 na hayati viongozi wa kiraia wa San Francisco na wahisani Richard na Rhoda Goldman. Washindi wa tuzo huchaguliwa na baraza la kitaifa kutoka kwa mapendekezo ya siri iliyowasilishwa na mtandao wa ulimwenguni wa mashirika ya mazingira na watu binafsi.

# # #